Kikapu

JKT Kikapu yaanza usajili wa kishindo

DAR ES SALAAM:Timu ya kikapu ya JKT imeanza maandalizi ya msimu mpya huku ikiendelea kutangaza usajili wake kwa ajili ya kujiandaa na Ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Ligi ya Taifa.

Kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii, JKT imetangaza usajili wa wachezaji watatu hadi sasa ambao ni Guardian Angel, Baraka Sabibi na Khalifan Mabrouck.

Guardian Angel alikuwa akiichezea Mchenga kabla ya kujiunga na JKT, Sabibi ametokea Pazi, huku Khalifan akitoka Vijana.

JKT ni miongoni mwa timu zinazofanya vizuri kwenye ligi za ndani na nje ya nchi, kwani imekuwa ikiwakilisha Tanzania kwenye Ligi ya Kikapu ya Kanda ya Tano Afrika na michuano mingine ya Afrika kila mwaka.

Kujiimarisha kwao huenda ni ishara ya nia ya kurejea kwa kishindo, kwa kuhakikisha wanakuwa na kikosi thabiti kitakachoweza kushindana na wapinzani wakali kama Dar City na UDSM Outsiders waliotoa ushindani mkubwa msimu uliopita.

Related Articles

Back to top button