Graham Potter kocha mtarajiwa Chelsea

KLABU ya Chelsea ‘The Blues’imefikia makubaliano na kocha wa Brighton & Hove Albion Graham Potter kuwa kocha mpya wa The Blues kufuatia kutimuliwa kazi kwa Thomas Tuchel.
Mjerumani huyo amekufukuzwa kazi Septemba 7 saa kadhaa baada ya Chelsea kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Dinamo Zagreb katika mchezo wa makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Ripoti zimesema Potter leo amekubali kwa maneno kuchukua nafasi hiyo.
Hakuna mkataba uliosainiwa lakini pande hizo mbili zimefikia makubaliano na Chelsea iko tayari kulipa ada ya kuondoka inayotakiwa kumwondoa kocha huyo kutoka Brighton.
Kwa mujibu wa ripoti Potter anatarajiwa kuiongoza Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Fulham Septemba 9.
Mapema leo Potter alikuwa kwenye uwanja wa mazoezi wa Brighton lakini hakuongoza mazoezi ya timu hiyo.
Ada inayotarajiwa kuliptwa Brighton kwa ajili ya fidia ni karibu pauni milioni 16 sawa na shilingi bilioni 42.3.