Africa

Gamondi:Kesho mtafurahi mbona!

ZANZIBAR: Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya CBE ya Ethiopia kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika mchezo utakaopigwa Uwanja wa New Amaan Zanzibar.

Kocha huyo amesema tayari amesahau matokeo ya mchezo uliopita na sasa nguvu zote zipo kwenye mchezo wa kesho huku akitamba kuwa amewaandaa vyema wachezaji wa timu hiyo na anaamini watafurahi baada ya dakika 90.

“Mechi iliyopita kweli tulikosa nafasi nyingi, Lakini kama kocha kukosa nafasi hutokea, muhimu ni kuwa na timu yenye uwezo wa kutengeneza nafasi nyingi, ukweli ni lazima kesho tutumie nafasi tunazopata,” amesema Gamondi.

Ameongeza kuwa hataki kuwapa wachezaji wake ‘presha’ kisa walikosa nafasi nyingi, anajua watacheza kwa utulivu lakini muhimu ni kuhakikisha wanatumia nafasi wanazopata.

“Hali ya wachezaji wangu ni nzuri, tumejiandaa vizuri sana na tumepata muda wa kujiandaa, nina wachezaji wakubwa sana wanaweza kufanya jambo bora kuliko wapinzani wetu, wachezaji wangu wanafahamu umuhimu wa kufuzu hatua ya makundi,” amesema kocha huyo.

Kwa upande wake mchezaji wa timu hiyo, Ibrahim Bacca amesema wanashukuru Mungu asilimia kubwa wachezaji wapo salama.

Amesema wamefanya mazoezi ya mwisho na matuamini yao kumaliza salama, anafuraha kubwa sana mchezo huo kufanyika Zanzibar ambapo ni nyumbani kwake huku akiwaahidi furaha mashabiki wa Yanga.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button