FA

‘Fainali CRDBFC mzigo mzito’ – Gamondi

DAR ES SALAAM. KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema licha ya kuwa na msimu mzuri bado wana kazi ngumu mbele yao katika fainali ya kombe la Shirikisho la CRDB Bank dhidi ya Azam FC.

Kikosi cha Yanga kimeondoka leo kuelekea Visiwani Zanzibar na ajili ya fainali hiyo ambayk watakuwa ugenini mbele ya wenyeji Azam FC, mchezo utakaochezwa Juni 2, mwaka huu uwanja wa New Amaan Complex, Visiwani Zanzibar, saa 2:15, usiku.

Akizungumza na SpotiLeo Gamondi amesema anafurahi kufikia malengo yao kwa kutwaa taji la ubingwa wa ligi pamoja na mchezaji wake Stephane Aziz Ki kufanikiwa kumaliza msimu akiwa kinara wa ufungaji bora.

“Licha ya yote lakini bado hatujamaliza kazi kubwa iliyopo mbele yetu ni fainali, Azam FC wako vizuri tunatakiwa kuwa makini kuhakikisha tunafanikiwa kushinda mechi hiyo,” amesema Gamondi.

Amesema wana fainali ya Shirikisho dhidi ya Azam FC, hautakuwa mchezo rahisi anaimani na vijana wake kufanya vizuri na kufanikiwa kutwaa taji hilo wakicheza vizuri na kufuata maelekezo yao.

“Msimu huu tumecheza vizuri, nimekuwa na timu bora, safu ya ulinzi, viungo na washambuliaji ksa kufanikiwa kuchukuwa tuzo ya ufungaji bora sasa tunaelekeza nguvu kwenye fainali yetu dhidi ya Azam FC.

Fainali ni timu mbili kati ya hizo lazima mmoja apate ushindi. Yanga kwangu ni timu bora kwa hapa nchini na tunaenda kucheza fainali kwenye uwanja mzuri ambao unachezeka vizuri,” alisema kocha huyo.

Gamondi ameeleza kuwa hautakuwa fainali rahisi kulingana na mechi ya mwisho walipokutana na Azam FC, walipoteza hali ambayo hataki kuona inajirudia katika fainali hiyo.

Yanga ilipoteza na kukubali kichapo cha mabao 2 -1 mbele ya Azam FC, mchezo wa Ligi Kuu Bara, Machi 17, mwaka huu, uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button