Bundesliga
Dortmund yamtimua Nuri Sahin

Borussia Dortmund wamemfuta kazi kocha wao Nuri Şahin baada ya miezi saba tu. Uamuzi huu umetangazwa leo Januari 22,2025, saa chache baada ya kufungwa 2-1 na Bologna kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya
Şahin aliteuliwa majira ya kiangazi akitokea kuwa msaidizi wa Edin Terzić msimu uliopita, lakini mambo hayakwenda vizuri. Dortmund wameshinda mechi 12 pekee msimu huu, huku kipigo dhidi ya Bologna kikiwa cha nne mfululizo.
Kocha wa zamani wa Ajax na Manchester United, Erik ten Hag, pamoja na Roger Schmidt, wanatajwa kuwa miongoni mwa wanaoweza kuchukua nafasi ya Şahin.