Davido amfikisha mahakamani mzazi mwenzie
MSANII wa Nigeria, David Adeleke ‘Davido’, amemfikisha mahakamani Sophia Momodu ambaye ni mama wa binti yake Imade, kwa kumtumia kujipatia fedha kupitia malezi.
Imeelezwa kuwa msanii huyo amedai apewe malezi kamili ya binti yake baada ya Sophia Momodu kumtumia kwa manufaa makubwa kupata fedha kutoka kwake.
Davido amemlalamikia mama wa Imade kuhitaji fedha nyingi na kukataa makubaliano waliyojiwekea ikiwemo kutekeleza majukumu ya kumtunza mtoto huyo.
“Sophia alikataa nyumba ya Naira milioni 200 (TZS mil. 350.3) yenye bwawa la kuogelea niliyonunua kwa ajili ya binti yangu Imade lakini alikataa.
Anataka niwe namlipia kodi ya Naira 5M (TZS mil. 9) kila mwaka, niwe namlipa mfanyakazi wake wa nyumbani dola 800 (TZS mil. 2.1) kwa mwezi na kutuma dola 19,800 (TZS milioni 51.6) kila mwaka kama pesa za matumizi kwa mtoto,” ameeleza Davido.
Davido ni mwimbaji wa Nigeria, mtunzi wa nyimbo na mtayarishi anayechukuliwa kuwa mmoja wa wasanii muhimu zaidi wa Afrobeats wa karne ya 21 kwa kufanya vizuri katika tasnia hiyo.