Muziki

Diamond, Nigeria na Afrika Kusini watawala uteuzi wa tuzo za MTV

LAGOS: MASTAA kadhaa wa Kiafrika wameteuliwa kuwania Tuzo za Muziki za MTV Europe (EMAs) 2024.

Katika kipengele cha Best African Act, walioteuliwa ni pamoja na Wanaijeria, Ayra Starr na Asake, Diamond Platnumz kutoka Tanzania, mkali wa Afrika Kusini Tyla, na DJ aliyegeuka mwimbaji DBN Gogo.
Wengine waliopo katika uteuzi huo ni mastaa wanaochipukia TitoM na Yuppe, wanaoshirikiana na ‘Tshwala Bam.’

Ayra Starr, Asake, Burna Boy, Tems na Tyla pia wamepata nafasi katika kipengele cha Best Afrobeats, ambacho kilijitokeza kwa mara ya kwanza kwenye tuzo hizo za EMA za mwaka jana ambapo Rema ndiye aliyetwaa tuzo hiyo mwaka 2023, na sasa anatetea taji hilo.

Tyla pia amechaguliwa kipengele cha Msanii Bora Mpya na Bora wa R&B huku Ayra Starr akiwa katika kipengele cha Msanii Bora Mpya.

Tuzo za MTV EMA za mwaka 2024 zitafanyika Manchester’s Co-Op Jumapili, Novemba 10. Mashabiki wanatakiwa kuwapigia kura wasanii wanaowapenda kwenye tovuti rasmi ya MTV EMAs, upigaji kura utasitishwa Novemba 6.

Related Articles

Back to top button