Kwingineko

Dembele aibua upya mjadala wa Balon D’or

ATLANTA, Paris St Germain wameinyuka 2-0 Bayern Munich na kutinga nusu fainali ya Kombe la Dunia la Klabu huku Ousmane Dembele akijumuisha utulivu wa kikosi cha Luis Enrique alipofunga ushindi wakati timu yake ilikuwa chini ya wachezaji tisa.

Dembele alifumania nyavu dakika ya sita ya muda wa nyongeza baada ya kutengenezewa kwa ustadi asisti kali na Achraf Hakimi na mshambuliaji huyo wa Ufaransa pia aling’aa kwa kujilinda kwa kuzuia bila kuchoka na kuanzisha mpira uliopelekea bao lake.

“Ningempa Ballon d’Or Ousmane Dembele. Jinsi anavyojua kulinda…ni hiyo pekee ndiyo inaweza kuwa na thamani ya Ballon d’Or. Hivi ndivyo unavyoongoza timu.” – kocha Luis Enrique alisema baada ya ushindi wa fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya Inter Milan.

Dembele alithibitisha hilo kwa kocha Enrique kwa mara nyingine tena dhidi ya Bayern jana. Alipumzishwa kwenye hatua ya makundi baada ya kupata jeraha la paja na akitokea tu baada ya mapumziko katika hatua ya 16 bora na katika robo fainali, Dembele alileta nguvu ya ajabu kwa timu iliyokuwa ikitawaliwa na Bayern.

PSG, inayosaka mataji mara nne baada ya kushinda Ligi ya Mabingwa, Kombe la Ufaransa na taji la Ligue 1, itamenyana na Real Madrid kuwania nafasi ya kucheza fainali.

Nahodha wa kikosi cha PSG Marquinhos hakuficha furaha yake na kuweka wazi kuwa wanataka kushinda taji hilo na kuiheshimisha klabu yake kwenye anga la soka duniani

“Ni wakati muhimu sana kwetu, tumefunga na kulipiza kisasi kwa Bayern baada ya fainali ya ligi ya mabingwa mwaka 2020 (Bayern alishinda 1-0) na baada ya kutufunga mapema msimu huu. Labda niseme tu tunataka kushinda shindano hili” alisema Marquinhos

Related Articles

Back to top button