Kuogelea

Delbert ampiku Collins michuano ya Kuogelea

MUOGELEAJI Delbert Ipilinga ameanza vizuri michuano ya wazi ya Taifa ya Kuogelea katika mtindo wa Breast mita 200 baada ya kushika nafasi ya kwanza na kuwapikU wapinzani wake Collins Saliboko, Shirashi Koji, Barreto Enrico na Fernandez Christian.

Katika michuano hiyo iliyoanza kwenye bwawa la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) Dar es Salaam Leo imeshirikisha wachezaji 238 kutoka Tanzania, Kenya na Uganda.

Akizungumza na Spoti Leo baada ya kumalizika kwa awamu ya kwanza ya mtindo huo, Delbert alisema anafurahi kufanya vizuri kwani ameweka rekodi yake ya Kuogelea dakika 2:38.

“Ushindi huu umetokana na mazoezi niliyofanya kwa muda mrefu, nilivyoingia kwenye maji nilijisikia mwepesi, nashukuru Mungu kwa upinzania mkal, umenisaidia kuongeza kiwango na kuwashinda wenzangu,”alisema.

 

Amesema ameweka rekodi mpya kwasababu mara ya mwisho Kuogelea aliogelea kwa muda wa dakika 2:40 hivyo ameboresha muda wake kwa kufanya vizuri.

Mwenyekiti wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA) David Mwasyoge  amesema mashindano hayo ni kalenda yao ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na mashindano ya kimataifa yajayo.

Amesema mwaka huu kumekuwa na ongezeko kubwa la wachezaji tofauti na mwaka uliopita ikionesha hamasa na mwamko umekuwa mkubwa.

Mashindano hayo yameshirikisha klabu 16, kati ya hizo, 14 ni kutoka Tanzania na klabu mbili ni kutoka Kenya na Uganda.

Klabu zilizoshiriki ni pamoja na Champion Rise, Premier, MSC,  Wahoo, Taliss, Sea horses, Bluefin, Dar Swim, Braeburn sharks, Riptide, Morogoro, Pigec, Braeburn Arusha, Lake Victoria na FK Blue Marlins

Related Articles

Back to top button