Daz Nundaz wapo mzigoni leo

Ikiwa ni miaka 25 tangu waanze kutumikia tasnia ya Bongo fleva kwa kuonesha kuwa bado wana nguvu ya kuendelea kuwaburudisha watanzania Daz Nundaz ‘Daznunda Family’ wanatarajiwa kufanya burudani leo katika ukumbi wa Ware House Masaki Jijini Dar es salaam.
Katika usiku wa kuwapa heshima wakali waliotoa mchango kwenye Bongofleva (Bongo Flava Honors) lililoandaliwa na Msanii wa Hip Hop Joseph Mbilinyi ‘Sugu’
Sugu amesema kuwa hii inaonyesha jinsi gani sanaa ipo kwenye damu na bado wana uwezo mzuri wa kuwahudumia kwa kuwapa burudani watanzania.
“Lengo la tamasha hili ni kutoa heshima na kuwasherehekea Ma-Legend waliofanya vizuri katika tasnia ya muziki Bongo fleva ambapo zamu hii ni ya Daz Nundaz.
Kundi linaloundwa na wakali kibao akiwemo Ferooz, Daz Baba, La’Rhumba , Sajo na Critic ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika muziki wa Tanzania.
Wasanii hao wamejipanga kushusha burudani kwa kutumia vifaa vya bendi mubashara, wakiwakumbusha mashabiki ngoma zao kali kama barua, Kamanda, nipe tano na zingine nyingi.