Africa

Coastal Union: Tutapindua meza kibabe

DAR ES SALAAM: WAWAKILISHI wa Tanzania katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Coastal Union kesho watashuka katika Dimba la Azam Complex wakiwa na matarajio makubwa ya kufanya vizuri katika mchezo wa marudiano wa awali wa mashindano hayo dhidi ya F.C. Bravos do Maquis ya Angola.

Coastal Union wanaingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa idadi ya mabao 3-0 nchini Angola .

Kuelekea mchezo huo Coastal itakuwa chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Ngawina Ngawina amesema licha ya kuwa na mlima mkubwa katika mchezo wa marudiano wamejiandaa kutafuta ushindi.

Amesema ana imani na vijana wake baada ya kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo wa kwanza na kupambana kutafuta ushindi wa mabao 4-0 ili kusonga mbele.

“Tumejipanga vizuri , hatuna majeraha hata mmoja, mpira ni dakika 90 , kama wao wamepata mabao 3-0 kwao na sisi tunaweza kufunga 4-0 Tanzania,” amesema Ngawina.

Ameongeza kuwa atafanya mabadiliko ya kikosi kwa mchezo wa kesho na ana imani vijana wako vizuri katika mapambano ya kusaka ushindi.

 

Related Articles

Back to top button