Bei ya Mason Mount bil 202.6/-

KLABU ya Chelsea imesema timu zenye nia ya kumsajili Mason Mount msimu huu wa majira ya joto zitalipa pauni milioni 70 sawa na shilingi milioni 202.6.
Hatma ya mchezaji huyo wa kimataifa wa England katika klabu ya Chelsea ipo shakani huku bado pande hizo hazifikia makubaliano ya kuongeza mkataba wake wa sasa unaomalizika mwisho wa msimu ujao.
Liverpool na Manchester United ni miongoni mwa klabu za Premier League zenye nia ya kumsajili Mount mwenye umri wa miaka 24.
Ripoti zimesema kocha mpya wa Bayern Munich Thomas Tuchel pia na nia ya kuungana kiungo huyo.
Chelsea inakusudia kukusanya fedha msimu huu wa majira ya joto baada ya kutumia pauni milioni 600 sawa na shilingi trilioni 1.7 kusajili wachezaji tangu dirisha la uhamisho la majira ya joto.