Nyumbani

Chaba wa Wahdzabe alalamikia watu wanaomtumia mitandaoni bila ridhaa yake

ZANZIBAR:MWMBAJI maarufu kutoka jamii ya Wahadzabe, Chaba, ameeleza masikitiko yake kuhusu baadhi ya watu wanaotumia jina, picha na video zake kwenye mitandao ya kijamii bila kumhusisha wala kumpatia manufaa yoyote.

Akizungumza wakati wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar, ZIFF 2026, Chaba alisema amekuwa akiona maudhui mengi yanayosambazwa mtandaoni yakimhusisha yeye na maisha ya jamii ya Wahadzabe, lakini mara nyingi wahusika wanaonufaika na maudhui hayo si watu wa jamii yake.

Chaba alisema umaarufu wake umechangia kuitangaza jamii ya Wahadzabe duniani, lakini bado kuna changamoto ya watu kutumia picha na video zake kwa ajili ya kujitengenezea kipato bila kupata kibali au kushirikisha jamii husika katika faida zinazotokana na maudhui hayo.

Kauli yake imeibua mjadala miongoni mwa washiriki wa ZIFF 2026 kuhusu haki za maudhui ya kidijitali, utamaduni na namna jamii za asili zinavyoweza kunufaika na umaarufu unaotokana na matumizi ya mitandao ya kijamii.

Chaba, ambaye amepata umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania kupitia video zinazoonesha maisha na utamaduni wa Wahadzabe, amekuwa mmoja wa sura zinazotambulika zaidi katika kuitangaza Tanzania kupitia urithi wa utamaduni wa asili.

Related Articles

Back to top button