Kwingineko

Bingwa wa Choreografi kusakwa Rotterdam nchini Uholanzi

ROTTERNDAM: SHINDANO la Kimataifa la Rotterdam ‘Duet’ Choreografi (RIDCC) linalohusisha watu wanaocheza kwa mfanano linawaalika wanaocheza kwa mfanano kutoka kote duniani wawasilishe sinema zao za dakika 7 hadi 12 wakiwa wanacheza ili wachaguliwe kwa ajili ya shindano hilo.

Shindano hilo la 7 litafanyika huko Rotterdam nchini Uholanzi kuanzia Juni 11 hadi 14 mwaka huu wa 2025.

Washiriki 16 tu ndiyo watakaoshiriki tamasha hilo baada ya mchujo wa awali na wataruhusiwa kuwasilisha maonesho yao ya moja kwa moja kwenye ukumbi wa michezo huko Rotterdam na yataonekana moja kwa moja duniani kote.

Mashindano ya mchujo wa awali yanawasilishwa wakati wa raundi za awali Juni 12 na 13. Juni 14, hafla hiyo itafungwa kwa fainali kwa washiriki kwa kushindanisha washiriki waliopita katika hatua zote za awali.

Baada ya fainali kamati ya tuzo itachagua mshindi wa Tuzo wa jumla na kamati ya RIDCC itachagua mshindi wa Tuzo za Washiriki kutoka kwa washiriki wote kumi na sita.

Katika mashindano hayo pia mtazamaji wamewekewa tuzo yao inayoitwa Tuzo ya Watazamaji msanii anayetaka kushiriki tuzo hizo anatakiwa awasilishe kazi zake kabla ya Machi 1.

Kamati ya mashindano hayo imeeleza kuwa iko wazi kwa mitindo yote ya densi na washiriki wawasilishe maonesho yao yasiyozidi watu wawili.

Kamati ya RIDCC itashughulikia malazi ya hoteli pamoja na kifungua kinywa kwa timu za wacheza densi na gharama za usafiri zitarejeshwa kwa kila mshiriki.

Related Articles

Back to top button