BIEN: Mke Wangu Chiki ndiyo nguzo yangu

KENYA: MWANAMUZIKI wa Kenya anayetamba na wimbo wa ‘Nairobi’ alioshirikishwa na msanii Marioo, Bien amekiri kwamba Mke wake Chiki ndiye nguzo yake anayoitegemea kwa sababu humuinua kila anaposhindwa kujiamini katika jambo Fulani.
“Kama msanii, uaminifu ndio kila kitu. Unahitaji mtu unayeweza kumtegemea kusimamia mambo yako, maisha yako, na kazi yako,” amesema Bien akimsifia mkewe Chiki kuwa nguzo imara kwake katika kila magumu anayopitia.
Bien amesema wapo wasanii waafrika wanaofanikiwa wakisimamiwa na wanafamilia, ndiyo kitu pekee kilichoniondoa hofu ya kufanyakazi kwa karibu na mke wake Chiki.
“Unapochagua mwenzi sahihi wa maisha, kila kitu kingine huanguka mahali pake,
“Nilipokuwa peke yangu mwaka jana, nilipata wasiwasi, shaka, na Chiki alinisaidia kubadili mawazo yangu na alinionyesha mambo kwa njia tofauti,
“Sikuzote tunajadili biashara, lakini sio kazi tu ni maisha yetu kwa ujumla. Tunaweza kuwa kitandani usiku wa manane tukizungumza kuhusu jambo fulani, na kwa kweli tunafuraha,” ameeleza Bien.