Tetesi

Benzema yupo sana Madrid

“Nakubaliana na Karim, sio kila unachokiona kwenye Internet kina uhalisia, ana mkabata wa mwaka mmoja mpaka 2024 hakuna mashaka katika hilo.” Amesema kocha wa Real Madrid, Carlo Ancellotti wakati akifafanua taarifa za Karim Benzema kutimkia Saudia.

Mwishoni mwa wiki hii ziliibuka taarifa kuwa mshambuliaji huyo raia wa Ufaransa alifanya mazungumzo na Al-Ittihad ya Saudia Arabia ili kutimka Bernabeu. Hata hivyo Benzema alikanusha taarifa hizo.

Ancellotti amesema Benzema ataendelea kuwepo msimu ujao kutumikia muda wake uliobaki: “Hakuna wasiwasi katika hilo.”ameongeza Ancellotti.

Kocha huyo amezungumzia mustakabali wake klabuni hapo akieleza kuwa kila kitu kipo sawa na ataendelea kubaki Madrid.

“ Nina furaha sana kuendelea na tutajaribu kufanya vyema zaidi msimu ujao, wachezaji wengine wataondoka, kutakuwa na mabadiliko lakini timu itakuwa nzuri”.ameongeza Ancellotti.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button