Tetesi

Real yataka uamuzi wa Mbappé Januari

TETESI za usajili zinaonesha Real Madrid ipo tayari kumpa ofa ya dili fowadi wa kifaransa, Kylian Mbappé,24, ambaye mkataba wake Paris Saint-Germain unamalizika majira yajayo ya kiangazi lakini lazima afanya uamuzi ifikapo Januari 15, 2024.(AS – in Spanish)

Fowadi mbrazil,Richarlison, 26, ni mlengwa wa usajili katika vilabu vya ligi ya kulipwa Saudi Arabia lakini Tottenham huenda isimuuze mchezaji huyo chini ya pauni milioni 60 ilizoilipa Everton.(90 Min)

Tottenham inafikiria kumsajili beki wa Everton na England Ben Godfrey, 25, Januari 2024.(Talksport)

Liverpool imeanza harakati za kumsajili fowadi mdachi wa Benfica, 18, Kyanno Lorenzo Silva.(Football Insider)

AC Milan inajiandaa kumsajili kwa mkopo beki wa Poland anayekipiga Arsenal, Jakub Kiwior,23, huku kukiwa na sharti la kumnunua.(90 Min)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button