EPL

Benni McCarthy ampigia chapuo Luis Enrique Man United

NAIROBI: KOCHA wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, Benni McCarthy, amemtaja Luis Enrique wa Paris Saint-Germain (PSG) kuwa kocha ambaye angependa kumuona akiongoza Manchester United, lakini amesisitiza kuwa klabu hiyo inapaswa kuendelea kumuunga mkono Michael Carrick.

McCarthy, ambaye aliwahi kuwa kocha wa washambuliaji wa Manchester United kati ya mwaka 2022 na 2024, amesema Enrique ni miongoni mwa makocha wanaovutia zaidi kutokana na uwezo wake wa kiufundi na mafanikio yake.

Hata hivyo, anaamini kuwa itakuwa vigumu kwa kocha huyo wa Hispania kuondoka PSG kutokana na mazingira mazuri ya kazi na mradi unaoendelea kujengwa katika klabu hiyo.

Akizungumza na Sporty TV, McCarthy alisema:

“Kwangu mimi, kocha anayestahili zaidi ambaye ningependa kumuona Manchester United ni Luis Enrique, lakini hataondoka PSG. Kama ningekuwa yeye, nisingefanya hivyo. Wana fedha, lakini ungekuwa mtu asiye na busara kuacha kile kinachojengwa PSG na kuja Manchester United.”

Badala ya kuanza tena mchakato wa kutafuta kocha mpya, McCarthy ameitaka Manchester United kumpa Carrick muda, imani na mamlaka ya kuijenga timu kulingana na falsafa yake ya soka.

Amesema Carrick alifanya vizuri mwishoni mwa msimu uliopita na kwamba wachezaji wameonesha mwitikio mzuri wanapokuwa chini ya uongozi wake.

“Michael Carrick alifanya vizuri sana mwishoni mwa msimu uliopita. Hivyo, muunge mkono, muamini na mpe msaada anaohitaji, pamoja na wachezaji anaotaka kuwasajili. Wachezaji wanamwitikia na wanacheza vizuri chini yake,” alisema McCarthy.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button