Ligi Kuu
Kivumbi mtoano kubaki Ligi Kuu
TABORA United leo itakuwa mwenyeji wa JKT Tanzania katika mchezo wa kwanza wa mtoano kubaki Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
JKT Tanzania imeshika nafasi ya 13 huku Tabora United ikiwa ya 14 katika msimamo wa ligi hiyo iliyofikia tamati Mei 28.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram kuelekea mchezo wa leo Tabora United imesema: “𝐖𝐢𝐤𝐢 𝐍𝐲𝐢𝐧𝐠𝐢𝐧e, 𝑴𝒄𝒉𝒆𝒛𝒐 𝑴𝒘𝒊𝒏𝒈𝒊𝒏𝒆, 𝑴𝒂𝒍𝒆𝒏𝒈𝒐 𝑴𝒆𝒏𝒈𝒊𝒏𝒆.”
Nayo JKT Tanzania imesema: “Baada ya kelele nyingi ni muda wa kurudisha heshima💪🏽
JKT Tanzania🇹🇿 tutakuwa ugenini kupambana kuhakikisha Tabora United wanaenda Championship.”
Mchezo wa marudiano kati ya timu hizo utafanyika Juni 8 kwenye wa Meja Gen Isamuhyo, Mbweni Dar es Salaam.