Barca yaipigia hesabu kali Leganes

BARCELONA, Meneja wa vinara wa LaLiga Barcelona Hansi Flick, amesema hawataichukulia poa Leganes na wanatarajia upinzani mkali kutoka kwao watakapotembelea uwanja wa Estadio Municipal de Butarque kesho jumamosi wakati wenyeji wao hao watakapojipapatua kutoka mkiani mwa Ligi hiyo.
Barca watakuwa wakisaka fursa ya kutanua pengo la uongozi dhidi ya mahasimu wao Real Madrid kwa pointi 7 badala ya 4 zilizopo sasa huku kukiwa na mizunguko nane iliyosalia kwenye LaLiga na Flick anasema wantaka kuchukulia kila mchezo kwa usiriazi wa hali ya juu.
“Ni timu nzuri inayojua kulinda vyema na wanajua kushambulia kwa kushtukiza. ni lazima tuwe makini kwenye mchezo huu kwa sababu tunaongoza ligi hii na sasa ni lazima tuthibitishe hilo na wao ni lazima wajinasue kutoka kwenye janga la kushuka daraja ni mechi ngumu sana” – Flick amesema
Wakatalunya hao watakuwa wakitafuta kulipiza kisasi baada ya Leganes kuwachapa 1-0 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza Mwezi Desemba baada ya pia kuwachakaza vigogo wengine wa LaLiga Atletico Madrid mwezi Januari na almanusura wawashangaze Real Madrid kabla ya kupoteana dakika za usiku na kupigwa 3-2 mwezi machi.