Nyumbani
Azam FC yashusha kocha la boli kutoka Morocco
DAR ES SALAAM: Klabu ya soka ya Azam FC imemtangaza kocha mkuu mpya Rachid Taoussi raia wa Morocco kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Kocha Taoussi, amekuja nchini na wasaidizi wake watatu, Kocha msaidizi, Ouajou Driss, Kocha wa utimamu wa mwili, Badr Eddine na Kocha wa makipa, Rachid ElI Mekkaoui.
Taoussi anachukua nafasi ya Yousouph Dabo ambaye aliachana na Azam FC hivi karibuni baada ya tetesi za muda mrefu kutokana na mwanzo mbaya wa klabu hiyo katika ngao ya jamii na michuano ya kimataifa ya CAF.
Kocha huyo ambaye ni kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Morocco amewahi kufundisha vilabu vikubwa vya nchini humo vikiwemo RSB Berkane, AS Far Rabat, Wydad Casablanca, CR Belouizdad.