Nyumbani

PM kushuhudia tuzo BMT

DAR ES SALAAM: WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi usiku wa tuzo za Wanamichezo bora zitatakazofanyika Juni 9, 2023, ukumbi wa Super Dome, uliopo Masaki, Dar es Salaam.

Akizungumza na Spotileo, Katibu Mtendaji Mkuu wa Baraza la Michezo Taifa (BMT), Neema Msitha amesema maandalizi yanaendelea vizuri kuelekea tuzo hizo na Waziri Mkuu atakuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.

Amesema kuna tofauti kubwa kati ya mwaka jana na mwaka huu na kuwa kimeongezwa kipengele cha wanahabari bora wa kiume na kike kwa kutambua mchango wao katika tasnia hiyo.

Miongoni mwa wanahabari anayewania tuzo hiyo ni mfanyakazi wa kampuni ya TSN inayochapisha magazeti ya Spotileo, Habari Leo, Daily News na Daily New Digital, Antipas Kavishe, akishindanishwa na Hosea Mchopo (ITV), Hussein Shafii (TBC) na Mahmoud Zubeir wa Azam TV.

“Mabadiliko haya yanalenga kuongeza ushindani na ufanisi ikiwa ni pamoja na kuleta usawa wa uthamani kwa michezo yote,kadhalika mabadiliko haya yataongezea thamani tuzo hizi.

Kuongezeka vipengele vingine ambavyo kwa mwaka jana havikuwepo baadha ya vipengele vilivyoongezeka ni pamoja na Kocha bora wa mwaka, Mwamuzi bora wa mwaka, Lengo la maboresho haya ni kuendelea kuhakikisha kuwa wadau wote muhimu katika tasnia ya michezo wanathaminiwa na kutambuliwa,” alisema Msitha.

Aliongeza kuwa Mabadiliko ya vipengele vya tuzo yamefanyika ili kuendelea kuipa thamani tuzo hizi zinazotolewa pamoja na kuongeza ushindani baina ya wanamichezo anayepewa tuzo awe ni yule ambaye amekuwa na mafanikio zaidi kuliko wanamichezo wengine wote.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button