LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja kufanyika Coastal Union ikiwa mwenye wa Kagera Sugar kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.
Coastal Union inashika nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 13 baada ya michezo 12 wakati Kagera Sugar ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 13 baada ya michezo 10.
Katika kipindi cha miaka sita timu hizo zimekutana mara 10 Coastal ikishinda mara nne, sare mbili na Kagera Sugar ikishinda mara nne.