Ariana kutoka muziki wa Pop hadi uigizaji
NEW YORK: MWANAMUZIKI Ariana Grande ameweka wazi kwamba anafahamu mipango yake ya kuingia katika uigizaji itawashangaza mashabiki wake lakini hatoacha muziki.
Nyota huyo wa ‘Wicked’ amesema jukumu lake la kuigiza kama ‘Glinda’ katika filamu kubwa yenye sehemu mbili ya ‘Broadwa Classic’ limemfanya atake kurejea katika misingi yake ya uigizaji lakini amewaahidi mashabiki zake kwamba hataachana na muziki.
Akitokea kwenye podikasti ya ‘Las Culturistas’, Ariana ambaye ametoa albamu saba tangu mwaka 2013 amesema anaogopa kutisha mashabiki wake lakini hatoacha muziki hata akiingia kwenye uigizaji.
“Nitasema jambo litawatisha mashabiki wangu na kila mtu, lakini ninawapenda, na watashughulikia na tutakuwa wote milele.
“Siku zote nitafanya muziki, nitapanda jukwaani, nitaimba pop, naahidi. Lakini sifikirii kuifanya kwa kiwango ambacho nimekuwa nikifanya kwa miaka 10 iliyopita ndipo ninapoona miaka yangu10 ijayo kuingia katika uigizaji.
Tasnia ya burudani ya mwanamuziki huyo wa pop mwenye umri wa miaka 31 ilianza kuonekana alipokuwa na miaka 15 tu mwaka 2008.
Ariana anayetamba na wimbo wa ‘Thank U, Next’ ambaye amepiga picha kwa kuigiza Paka Valentine maarufu katika mfululizo wa ‘Nickelodeon’ kutoka 2010 hadi 2013 amewahasa mashabiki wake kutokuwa na hofu nay eye kwa kuwa anaonyesha kipaji chake kingine.