Argentina yapokewa kishujaa
						BINGWA wa Dunia, Argentina imerejea nyumbani kwa kupokewa kishujaa na maelfu ya mashabiki baada ya kutua kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ezeiza jijini Buenos Aires kufuatia kutwaa ubingwa huo.
Argentina imetwaa ubingwa huo kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya sare ya mabao 3-3 dhidi ya Ufaransa katika muda wa nyongeza wakati wa michuano ya Kombe la Dunia Qatar 2022.
Timu hiyo ya taifa na taji la Kombe la Dunia ambalo imelitwaa kwa mara ya tatu Novemba 18 imetua Argentina majira ya saa 8.20 alfajiri leo baada ya safari ya karibu saa 21 angani.

Basi la mabingwa hao limepita mitaa ya Buenos Aires na mashabiki walifurika kwenye mitaa kuwaona mashujaa wao.

Fataki ziliangaza angani juu ya umati wa watu huku kikundi cha muziki cha ‘La Mosca’ kilicheza.

Mashabiki hao walipiga ngoma na kucheza wakati wakiendelea kusherehekea ubingwa wa timu yao katika hatua ya juu zaidi ya soka duniani.
				
					



