World Cup

Real Madrid ‘yamnawa’ Ancelotti

MADRID: Klabu bingwa ulaya Real Madrid imethibitisha itashiriki michuano Kombe la Dunia la Vilabu la FIFA linalotarajiwa kutimua vumbi Juni na Julai 2025 nchini Marekani

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye website ya klabu hiyo, Real Madrid imesema ushiriki wao katika mashindano ya FIFA haujawahi kuwa wa mashaka na kuthibitisha uwepo wao kwenye mashindano yajayo.

“Hakuna wakati wowote ushiriki wetu katika Kombe jipya la Dunia la Vilabu litakaloandaliwa na FIFA katika msimu ujao wa 2024/2025 umetiliwa shaka”.

“Tutakuwepo FIFA CWC kama tulivyopanga tutacheza kwa ari na kwa shauku kubwa ya kufanya mamilioni ya mashabiki wetu kote ulimwenguni kupata tena hamu ya kushinda taji jipya”, taarifa hiyo imesema

Kwa upande wake kocha mkuu wa kikosi cha Los Blancos Carlo ancelotti ameandika katika mtandao wake wa X na kusema kuwa mahojiano yake na gazeti la Il Giornale la Italy yaliyomnukuu kocha huyo kusema Real Madrid haitashiriki Vuta N’kuvute hiyo ya 2025 hayakutafsiriwa vizuri.

“Katika mahojiano yangu na Il Giornale, maneno yangu kuhusu Kombe la Dunia la Vilabu la FIFA hayajafasiriwa nilivyokusudia”, amesema Ancelotti

“Hakuna kinachozidi maslahi zaidi ya kukataa uwezekano wa kucheza michuano ambayo nadhani inaweza kuwa fursa nzuri ya kuendelea kupigania mataji makubwa na Real Madrid”. Alimaliza

Taarifa hii ya Real Madrid inakuja kama brashi kusafisha kauli ambayo ilizua utata ya Ancelotti ambapo awali alinukuliwa akisema klabu yake itakataa kushiriki kombe la dunia la vilabu 2025 linaloandaliwa na FIFA.

Related Articles

Back to top button