Kwingineko
Ander Herrera ajiunga na Boca JuniorsBUENOS

BUENOS AIRES:ANDER Herrera, kiungo wa zamani wa Real Zaragoza, Manchester United, na PSG, amejiunga rasmi na Boca Juniors baada ya kumaliza mkataba wake na Athletic Club.
Herrera ameingia mkataba wa mwaka mmoja na chaguo la kuongezwa mwaka mwingine, akihamia nje ya ligi tano bora za Ulaya kwa mara ya kwanza isipokuwa msimu mmoja akiwa Zaragoza (2008/09).
Herrera anatarajiwa kushiriki Kombe la Dunia la klabu, ambapo Boca itakabiliana na Bayern Munich, Benfica, na Auckland City.
Akiongea kuhusu uhamisho huo, alisema: “Boca ni klabu kubwa yenye historia na shauku ya kipekee. Nimewahi kuhisi uzuri wa La Bombonera kama shabiki, na sasa ninasubiri kwa hamu kuichezea.”