Nyumbani

Aly Mayai ashangazwa Samatta kustaafu timu ya Taifa

DAR ES SALAAM: Mchambuzi wa masuala ya soka, Aly Mayai, amesema ameshtushwa na uamuzi wa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, kutangaza kustaafu kuitumikia timu ya taifa, akieleza kuwa bado alikuwa na uwezo mkubwa wa kuendelea kuisaidia Tanzania katika mashindano ya kimataifa.

Akizungumza kuhusu uamuzi huo, Aly Mayai alisema Samatta ni mmoja wa wachezaji walioiletea heshima kubwa taifa kupitia kiwango chake yna uzoefu alioujenga ndani na nje ya nchi, hivyo anaamini mchango wake ungeendelea kuwa muhimu kwa kizazi cha sasa cha wachezaji.

Aliongeza kuwa licha ya kuheshimu uamuzi wa mchezaji huyo, anaona bado kulikuwa na nafasi kwa Samatta kuendelea kuitumikia Taifa Stars, hasa katika kipindi ambacho timu inaendelea kujijenga kuelekea mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Hata hivyo, Aly Mayai alimpongeza Samatta kwa huduma yake ya muda mrefu kwa Taifa Stars, akisema amekuwa mfano wa kujituma, nidhamu na uzalendo, huku akieleza kuwa historia yake itaendelea kukumbukwa kama mmoja wa wachezaji walioacha alama kubwa katika soka la Tanzania.

Related Articles

Back to top button