Africa

Ajali yaua shabiki wa Simba

MTU mmoja amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika ajali ya gari la mashabiki wa klabu ya Simba eneo la Vigwaza mkoa wa Pwani ikiwa ni moja ya ajali mbili zilizohusisha mashabiki wa timu hiyo.

Taarifa ya Simba imesema ajali hiyo imetokea wakati mashabiki hao wa tawi la Kiwira Rungwe mkoani Mbeya wakielekea Dar es Salaam kushuhudia mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya timu yao na Al Ahly ya Misri leo.

“Ajali ya pili ni tawi la wekundu wa border kutoka Tunduma iliyotokea Doma, mkoani Morogoro. Taarifa kutoka eneo la tukio inaeleza kuwa mtu mmoja ameumia na hakuna madhara makubwa,” imesema taarifa hiyo.

Mchezo kati ya Simba na Al Ahly utafanyika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button