Muziki

Bella ashusha ‘Rhumba Vol. 6’

DAR ES SALAAM: MSANII wa Muziki wa Dansi nchini Christian Bella ameachia albamu yake aliyoipa jina  la ‘Rhumba Volume One’ yenye nyimbo 6 alizoimba na bendi yake ya Malaika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Christian Bella amesema albamu hiyo ameandaa kwa lengo la kuburudisha na kuupa heshima muziki wa dansi.

“Albamu ya Rhumba Volume One inanyimbo nzuri na leo nimeachia rasmi ipo kwenye platform zote unaweza kusikiliza na kufurahia muziki wa Rhumba wa aina yake.

“Kubwa ni kurudisha muziki wa Rhumba kwenye hadhi yake kama ulivyokuwa ukifanya vizuri awali kwa kuwafikia mashabiki wa rika lote.

“Nimefanya albamu mbili Rhumba Volume One na two ambayo zote zina nyimbo 6 ujumla 12 ambapo ya kwanza nimefanya na bendi yangu ya Malaika Band na albamu ya pili nimeimba na wasanii mbalimbali wakiwemo wa Bongo fleva pamoja na hip hop.”amesema

Bella ambaye hivi karibuni aliachia albamu yake inayoitwa ‘Utaniuwa’ inayofanya vizuri YouTube amesema kuwa hali ya muziki imebadilika kwa sasa watu wanaangalia matokeo na mauzo ya kazi uliyofanya.

Pia ameeleza sababu ya kufanya kazi na wasanii wa Bongo fleva, Hip hop na Taarabu ni kutaka kuwateka mashabiki wa muziki huo waupende muziki wa Dansi.

Related Articles

Back to top button