Africa
Jeshi la Yanga dhidi ya Al-Merrikh

KLABU ya Yanga imetangaza kikosi cha wachezaji kinachosafiri leo kwenda Rwanda kwa ajili ya mchezo wa kwanza kufuzu makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al-Merrikh Septemba 16.
Imewataja magolikipa kuwa ni Djigui Diarra, Metacha Mnata na Abutwalib Mshery.
Mabeki ni Dickson Job, Ibrahim Abdullah, Gift Fred, Kibwana Shomari, Mutambala Lomalisa, Nickson Kibabage na Kouassi Yao.
Viungo kwenye msafara huo ni Khalid Aucho, Jonas Mkude Zwadi Mauya, Mudathir Yahya, Slaum Abubakar, Farid Mussa, Chrispin Ngushi, Jesus Moloko, Denis Nkane na Mahlatse Makudubela.
Yanga imewataja mafowadi kuwa ni Maxi Nzengeli, Pacome Zouzoua, Stephane Aziz Ki, Clement Mzize, Kennedy Musonda na Hafiz Konkoni.