Tetesi

Arsenal, Bayern watoana damu kwa Rice

MCHUANO mkali unaendelea kati ya Arsenal na Bayern Munchen juu ya usajili wa kiungo Declan Rice kutoka West Ham.

Imeelezwa Arsenal tayari wamekubaliana na Mwingereza huyo kukamilisha dili hilo. Shirika la habari la Uingereza BBC limeunukuu mtandao wa Football Transfer.

Wakati taarifa hizo zikiwafikia Bayern, imefahamika kuwa wawakilishi wa Bavaria hao wamefanya mazungumzo ya siri na kiungo huyo huko London lengo ni kuangalia uwezekano wa kuwasilisha ofa kwa West Ham. Mtandao wa Sky Sport umeripoti kutoka Ujerumani.

Rice amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake msimu huu wa joto licha ya West Ham kuwa wana chaguo la kuongeza mwaka mwingine.

Rice alikataa ofa ya mkataba mpya wa pauni 200,000 kwa wiki miezi 18 iliyopita akiwa klabuni hapo, imeelezwa madai yake ni kucheza mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button