Africa
Simba karata muhimu CAF leo

KLABU ya Simba inajitupa dimba la ugenini la St Mary lililopo Kitende, Kampala, Uganda kuikabili Vipers ya nchi hiyo katika moja ya michezo mitano ya Ligi ya Mabingwa Afrika inayopigwa leo.
Simba inashika nafasi ya 4 mwisho wa msimamo wa kundi C baada ya michezo miwili ikiwa haina alama.
Katika Raja Casablanca inaongoza kundi hilo ikiwa na alama 6, ikifuatiwa na Horoya yenye alama 4 na nafasi ya 3 ipo Vipers yenye alama 1.
Michezo mingine ni kama ifuatavyo:
Kundi A
AS Vita Club vs JS Kabylie
Kundi B
Al Ahly vs Mamelodi Sundowns
Kundi C
Raja Casablanca vs Horoya
Kundi D
Esperance vs vs Zamalek