Africa
Yanga ugenini CAFCL leo
KLABU ya Yanga leo inashuka dimbani Algeria katika mchezo wa kwanza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kundi D dhidi ya CR Belouizdad.
Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa 5 July 1962 uliopo mjii mkuu wa nchi hiyo, Algiers.
Mchezo mwingine wa michuano hiyo leo ni wa kundi A ambapo Pyramids itakuwa uwanja wa nyumbani wa 30 June uliopo Cairo, Misri dhidi ya TP Mazembe.