Ighodaro mali ya Chippa United

KLABU ya Chippa United ‘Chilli Boys’ inayoshriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini imetangaza kumsajili mshambuliaji wa Nigeria, Etiosa Ighodaro.
Usajili wa Ighodaro mwenye umri wa miaka 21 ni wa 17 kwa Chilli Boys baada ya wachezaji 16 kutambulishwa katika klabu hiyo mwezi uliopita.
Ighodaro anatarajiwa kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya Chippa United.
“Tunafuraha kumkaribisha mshambuliaji hodari kijana kwenye klabu,”Ukurasa wa Twitter wa klabu hiyo umeandika.
Mwenyekiti wa Chippa United Siviwe Mpengesi ameiambia tovuti ya klabu hiyo kwamba Etiosa ni mfungaji mabao asilia ambaye hivi karibuni atakuwa kipenzi kikuu cha mashabiki wa timu hiyo.
“Nina furaha amechagua kujiunga nasi, kwa kuwa alikuwa anawaniwa na klabu nyingine,” amesema Mpengesi.