Kikapu

Dar City yaichapa Ferroviário Da Beira

NAIROBI: TIMU ya Dar City imeendeleza kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika mashindano ya kufuzu Ligi ya Kikapu Afrika (BAL) 2027 baada ya kuichapa Ferroviário da Beira ya Msumbiji kwa vikapu 96-76.

Dar City imepata ushindi huo katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Kasarani jijini Nairobi, Kenya Leo jioni ambako timu hiyo inashiriki hatua ya Elite 16, Kanda ya Mashariki.

Ushindi huo unaonesha ushindani wa Dar City katika hatua hiyo muhimu ya mashindano inayowakutanisha baadhi ya timu zinazowania nafasi ya kucheza hatua ya mwisho ya kufuzu BAL 2027.

Dar City imekuwa ikiiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo ikiwa na dhamira ya kufanya vizuri na kusaka nafasi ya kucheza Ligi ya Kikapu Afrika msimu ujao.

Related Articles

Back to top button