Fernandez agoma kuongeza mkataba mpya United

MANCHESTER: NAHODHA wa Manchester United, Bruno Fernandes, amekataa ofa ya pili ya mkataba kutoka klabu hiyo, huku mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.
Ofa ya kwanza ya klabu hiyo iliwasilishwa wakati wa kiangazi, mazungumzo ya mkataba mpya yalipoanza, lakini ilikataliwa na Fernandes.
Katika mkatana wake unaoisha sasa, United ina chaguo la kuongeza muda wa kiungo huyo, 32 kukaa Old Trafford kwa mwaka mmoja zaidi.
Msimu uliopita, Fernandes alikuwa akiwaniwa na baadhi ya ikiwemo ya Al Hilal ya Saudi Arabia.
Mazungumzo yanatarajiwa kuendelea kati ya Fernandes na United, huku klabu hiyo ikiweka wazi kuwa inataka nahodha wake huyo aendelee kubaki Old Trafford.
Fernandes alitunukiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa PFA mwezi Agosti, mwaka huu baada ya kutoa pasi 21 za mabao msimu uliopita na kuweka rekodi mpya katika Ligi Kuu ya England.
Haijafahamika kama ujio wa Mauricio Pochettino anayetarajiwa kutangazwa kuwa kocha mkuu mpya wa United siku ya Ijumaa, kufuatia kufukuzwa kwa Michael Carrick siku ya Alhamisi, kama ni chanzo cha Fernandez kutotaka kuongeza mkataba.
Aidha, Fernandez aliwahi kukiri kuwa mwaka 2019, alikaribia kujiunga na kocha huyo raia wa Argentina, kipindi ambacho Pochettino alikuwa Tottenham, lakini uhamisho huo ulizuiwa na klabu ya Sporting aliyokuwa akiitumikia wakati huo.




