Kwingineko

Kane apewa mkataba mpya, mshahara mnono Bayern Munich

MUNICH: MSHAMBULIAJI wa Bayern Munich, Harry Kane, amesaini mkataba mpya na klabu hiyo utakaomuweka Alianz Arena hadi Juni, 2029.

Mkataba huo mpya unakadiriwa kuwa na thamani ya Pauni milioni 25 kwa mwaka, kiasi ambacho ni zaidi ya Pauni 401,000 kwa wiki na kuwa mchezaji anayelipwa kiwango cha juu Ulaya.

Hiyo imekuja, siku chache baada ya Kane kutwaa Tuzo ya Ballon d’or, kufuatia kiwango bora anachokionesha tangu alipojiunga na Bayern akitokea Tottenham Hotspur mwaka 2023 kwa ada ya Pauni milioni 85.

Tangu ajiunge na mabingwa hao wa Ujerumani, nahodha huyo wa England amefunga mabao 156 katika michezo 161.

Baada ya kutangazwa kwa mkataba mpya, Kane, 33 alisema: “Ninahisi kama niko nyumbani kabisa hapa FC Bayern.

“Ninaipenda klabu hii, mashabiki wake, na jiji la Munich. Tuna timu nzuri sana, na pia tuna kocha mahiri, Vincent Kompany.

“Ninajivunia sana kuwa sehemu ya klabu hii. Familia yangu yote ina furaha kubwa hapa. Nilikuwa na hamu kubwa ya kubaki.

“Sasa ninatazamia yajayo, na ninataka kushinda mataji mengine mengi zaidi nikiwa na klabu hii kubwa.”

Related Articles

Back to top button