Mitindo

Mama Jihan: Mwanangu ni Mtanzania mwenye asili ya kisukuma

DAR ES SALAAM: MAMA mzazi wa Jihan Dimack, Shufaa Ismail, amefunguka kuhusu asili ya mwanaye baada ya kutwaa taji la Miss Grand International 2026, akisisitiza kuwa Jihan ni Mtanzania mwenye asili ya Kisukuma, aliyezaliwa na kusoma Mkoani Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Shufaa amesema uwezo wa mwanaye kuzungumza Kiingereza kwa ufasaha haupaswi kuwafanya watu kuwa na mashaka kuhusu asili yake.

“Mwanangu kazaliwa na kusoma Mwanza, ni Msukuma, labda kile Kiingereza ndiyo kinawachanganya,” amesema Shufaa.

Aidha, Shufaa ameeleza hisia zilizomkumba wakati Jihan alipotangazwa mshindi wa taji hilo nchini Thailand, akisema alijikuta akilia kwa nguvu na kubaki amezubaa kutokana na furaha na mshangao wa ushindi huo.

Amesema msisimko wa wakati huo ulimfanya presha yake kupanda na mwili wake kuvimba, akieleza kuwa ilikuwa ni hali iliyotokana na hisia kali alizopitia wakati wa tukio hilo.

Vilevile, Shufaa amesema safari yao nchini Thailand ilikuwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo kukesha usiku na kupata muda mchache wa kupumzika.

Kauli ya Shufaa imekuja wakati ushindi wa Jihan Dimack ukiendelea kuzungumziwa, huku mama yake akisisitiza utambulisho wake wa Kitanzania na asili yake ya Kisukuma.

Related Articles

Back to top button