Muziki

Mbabe wa R&B, Freddie Jackson afariki dunia

CALIFORNIA: GWIJI wa muziki wa R&B, Freddie Jackson aliyefahamika kwa sauti yenye nguvu na mvuto iliyoimba nyimbo kama You Are My Lady na Rock Me Tonight, amefariki dunia.

Familia ya Freddie imetangaza habari hizo za kusikitisha ikisema kuwa mwimbaji huyo alifariki juzi Jumatatu ambapo sababu ya kifo chake haijawekwa wazi.

Familia yake inamkumbuka Freddie, kama mtu aliyekuwa zaidi ya gwiji wa muziki, ikimtaja kama kuwa mwenye moyo mwema na ukarimu ambaye aliwapenda mashabiki wake, familia, marafiki, na muziki kwa moyo wake wote.

Waliongeza kwa kusema: “Kwa miongo kadhaa, alitupatia nyimbo zilizokuwa sehemu muhimu ya hadithi zetu za mapenzi, sherehe zetu, na kumbukumbu zetu za thamani zaidi. Kipaji hicho kitaendelea kuishi milele.”

Freddie, 70 alikuwa mmoja wa waimbaji mahiri na maarufu zaidi wa R&B katika miaka ya 1980, akitawala chati za muziki kwa nyimbo tamu za mapenzi kama You Are My Lady, Rock Me Tonight, Have You Ever Loved Somebody, Jam Tonight na nyingine.

Familia inasema kuwa taarifa kuhusu mipango ya mazishi na namna ya kuenzi urithi wa Freddie zitatolewa katika siku za usoni.

Related Articles

Back to top button