Filamu

Digger yaingiza milioni 424 nchini India,

....yashuka kwa asilimia 96

LOS ANGELES: Filamu mpya ya staa wa Hollywood, Tom Cruise, Digger, imeanza vibaya katika soko la sinema nchini India, baada ya kukusanya takribani Sh milioni 424 katika siku tatu za kwanza tangu kuanza kuoneshwa.

Kwa mujibu wa takwimu za Hindustan Times, filamu hiyo ilianza kwa kupata takribani Sh milioni 178 siku ya Ijumaa, sawa na rupia milioni 6.5, kabla ya mapato kushuka zaidi siku ya Jumamosi na kushuka zaidia siku ya Jumapili ambapo ilifikia jumla ya takribani Sh milioni 424 nchini India.

Matokeo hayo ni tofauti kubwa na filamu nyingine za Tom Cruise zilizowahi kufanya vizuri nchini humo. Ikiwemo ‘Mission: Impossible – The Final Reckoning’ ambayo ilikusanya zaidi ya Sh bilioni 2.7, huku ‘Top Gun: Maverick’ ikifikia karibu Sh bilioni 1.3 katika soko la India.

Hindustan Times imesema ‘Digger’ imeonesha kushuka kwa takribani asilimia 96 ikilinganishwa na kiwango ambacho ‘Top Gun: Maverick’ ilifikia katika siku zake tatu za kwanza nchini India.

‘Top Gun: Maverick’ ilikuwa imekusanya takribani Sh bilioni 10.4 katika siku tatu za mwanzo, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na chombo hicho.

Kwa upande wa soko la kimataifa, ‘Digger’ pia imeanza kwa kasi ndogo. Filamu hiyo imekusanya takribani Dola milioni 20 duniani katika siku tatu, huku ikikusanya karibu Dola milioni 8 katika wikendi yake ya kwanza huko Amerika Kaskazini.

‘Digger’ inamwonesha Tom Cruise akiwa katika nafasi ya mfanyabiashara tajiri wa mafuta ambaye vitendo vyake vinasababisha janga la asili, kisha analazimika kujaribu kuishawishi dunia kwamba yeye ndiye mwenye uwezo wa kuwaokoa. Filamu hiyo pia inawashirikisha Riz Ahmed, John Goodman na Sandra Hüller.

Licha ya baadhi ya waigizaji kusifiwa kwa uigizaji wao, filamu hiyo imekumbana na changamoto za mapokezi na maoni ya wakosoaji, jambo ambalo limeelezwa kuwa miongoni mwa sababu za kuanza kwake kwa kasi ndogo katika box office.

Related Articles

Back to top button