Mastaa

Sugu aweka wazi utajiri wake

DAR ES SALAAM: RAPA mkongwe, Sugu au Mr. II kama anavyofahamika amekanusha taarifa za kuwa na utajiri wa Dola milioni 50 mpaka 150.

Mtayarishaji huyo wa shoo za Bongo Fleva Honors amelieleza hilo leo Alhamisi na kubainisha kuwa utajiri alionao kwa sasa hauzidi Dola milioni 10 (sawa na Sh bilioni 26).

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Mtandao wa Instagram, Sugu aliweka picha kutoka mtandao ambao hakuutaja wenye maelezo juu ya utajiri wake.

Mtandao huo ulifafanua zaidi kuwa utajiri wa mkongwe huyo umetokana na uwekezaji, muziki, biashara na masuala ya siasa alipokuwa Mbunge wa Mbeya Mjini kuanzia mwaka 2010 mpaka 2020.

“Nimeikuta hii ‘online’ leo, yao sio ya kweli.
Utajiri wangu wa kweli pamoja na mke wangu Happiness Mbilinyi mpaka sasa hauzidi Dola milioni 10,” alisema Sugu au Joseph Mbilinyi.

Related Articles

Back to top button