Muziki
Natamba Nae ya Bosco yashtua mashabiki

DAR ES SALAAM: BAADA ya kimya cha muda mrefu, mwimbaji wa injili nchini, Kelvin Bosco anatarajia kurudi kivingine na wimbo, Natamba Nae, mapema mwezi ujao.
Kelvin Bosco, ameweka wazi kuwa tangu alipotangaza ujio wa wimbo huo, amepokea shauku nyingi kutoka kwa mashabiki mtandaoni wanaosubiri kwa hamu ujio wake mpya.
Akizungumza na SportLeo, Kelvin Bosco alisema wimbo huo ni mwendelezo wa kumsifu Mungu na kuonyesha umhimu wa kutamba na uwepo wa Mungu kwenye maisha.
“Wimbo utatoka Oktoba 1, katika mitandao yote ya muziki, naamini nitawashtua mashabiki zangu ambao wanenisubiri muda mrefu sana, naomba wakae mkao wa kuhudumiwa na wimbo huu,” amesema Kelvin Bosco.




