Muziki

Macklemore azindua ziara ya Free Palestine

NEW YORK: RAPA Macklemore amezindua ziara yake ya muziki aliyoipa jina la Free Palestine, baada ya kutemwa kwenye Loop Tour ya Ed Sheeran.

Mackle amebainisha kufanya hivyo akidai amepata muda mwingi bila ya kufanya kazi kutokana na kuvurugika kwa ratiba yake baada ya kutemwa kwenye Loop Tour.

Kutemwa kwake Loop Tour kulitokana na maneno yake mafupi ya: “Free Palestine”, aliyoyasema wakati akitumbuiza kwenye jukwaa la ziara hiyo huko New Jersey na kutowafurahisha waandaaji wa shoo hiyo, walioamua kumuweka pembeni.

Mtandao wa BBC umeripoti ziara hiyo itaanzia Dublin mnamo Oktoba 26 kisha Oktoba 29 itafanyika Paris na London itakuwa Oktoba 30, mwaka huu.

“Wiki chache zilizopita zimenionesha kuwepo kwa mwamko wa pamoja kuhusu ukombozi wa Palestina, nguvu za mabilionea wanaojaribu kuzima wito huo, na yale tunayotarajia kutoka kwa wasanii kwa sasa.

“Kilichonipata ni kikubwa zaidi ya msanii mmoja au jukwaa moja. Wakati tabaka la mabilionea linapoamua ni sauti zipi zinaruhusiwa kusikika jukwaani na zipi ni hatari mno kusikika, kila mtu anapaswa kuwa makini na kufuatilia jambo hilo,” alisema Macklemore.

Amesema wiki iliyopita aliwasiliana na wasanii waliotumia majukwaa yao kuonesha mshikamano na watu wa Palestina, bila kujali matokeo yake na kwamba taarifa zaidi zitafuata ikiwemo ratiba za atakapopitisha ziara yake katika miji ya Marekani pia.

Aidha, amebainisha kuwa mapato yatakayotokana na ziara hiyo, yataelekezwa kwa mashirika yanayowaunga mkono Wapalestina.

Related Articles

Back to top button