Priyanka Chopra asherehekea miaka 34 ya mumewe Nick Jonas

LOS ANGELES: MWANAMUZIKI Nick Jonas ameadhimisha kutimiza miaka 34, huku mkewe, mwigizaji Priyanka Chopra, akitumia siku hiyo kumtumia ujumbe wa pongezi na kumshirikisha katika kumbukumbu za familia yao.
Priyanka alishiriki ujumbe huo pamoja na picha inayomuonesha Nick akiwa na binti yao Malti, hatua iliyovuta hisia za mashabiki na wafuasi wa wawili hao kwenye mitandao ya kijamii.
Ujumbe huo umeonesha upande wa kifamilia wa mastaa hao, ambao wameendelea kushirikisha baadhi ya matukio yao muhimu na mashabiki kupitia mitandao ya kijamii.
Nick Jonas, ambaye ni mwanachama wa kundi la Jonas Brothers, ameendelea kujenga jina lake katika muziki huku pia akijihusisha na shughuli mbalimbali za burudani.
Kwa upande wake, Priyanka Chopra ni mmoja wa waigizaji wanaotambulika kimataifa, akiwa amefanya kazi huko Bollywood na Hollywood.
Ujumbe wa Priyanka kwa Nick umeendelea kuwa miongoni mwa habari zinazozungumziwa katika ulimwengu wa burudani, hasa kutokana na picha ya Nick akiwa pamoja na binti yao Malti.




