Mastaa

Ziara ya ED Sheeran na Macklemore yazua zogo

LOS ANGELES: Ziara ya kimuziki ya mwanamuziki maarufu Ed Sheeran imeingia kwenye mjadala baada ya mabadiliko ya kushangaza kutokea kwenye orodha ya wasanii waliokuwa wamepangwa kuungana naye, huku jina la rapa Macklemore likiondolewa na wasanii wengine wakidaiwa kujiondoa kwenye mpango huo.

Mbali na Macklemore, wasanii wengine waliokuwa wamepangwa kushiriki kama wasanii wa ufunguzi pia wameripotiwa kujiondoa, hali iliyoongeza mjadala kuhusu mabadiliko yanayoendelea katika ziara hiyo.

Kutokana na hali hiyo, Ed Sheeran ameshirikiana na kampuni ya Guitar Center kuanzisha shindano la ‘Open for Legends’, linalolenga kumpata msanii mwingine atakayepata nafasi ya kufungua baadhi ya matamasha yake.

Hatua hiyo imeendelea kuvuta hisia katika tasnia ya muziki, huku mjadala ukiangazia mabadiliko katika ratiba ya ziara hiyo na nafasi ya wasanii wanaochaguliwa kufungua matamasha ya wasanii wakubwa.

Kwa sasa, ‘Open for Legends’ imekuwa sehemu ya hatua zinazochukuliwa kutafuta msanii mpya wa kupewa nafasi hiyo, wakati mjadala kuhusu mabadiliko yaliyotokea katika ziara ya Ed Sheeran ukiendelea.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button