Kwingineko

Manchester United yatolewa Carabao Cup

England: Manchester United imeondolewa kwenye michuano ya Carabao Cup baada ya kupoteza kwa mabao 3–2 dhidi ya Brighton & Hove Albion, katika mchezo wa kusisimua uliochezwa usiku wa kuamkia leo Septemba 17, 2026, kwenye Uwanja wa Old Trafford.

United ilianza kwa kasi kubwa na kupata mabao mawili ndani ya dakika 10 za kwanza.

Shea Lacey aliifungia United bao la kwanza, kabla ya Mason Mount kuongeza la pili na kuifanya timu hiyo ionekane ikiwa kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele.

Hata hivyo, Brighton ilifanya mrejesho mkubwa na kuanza kuibadilisha hali ya mchezo. Charalampos Kostoulas alifunga bao la kwanza la Brighton mwishoni mwa kipindi cha kwanza, kabla ya Pascal Gross kusawazisha katika dakika ya 65.

Dakika nne baadaye, Maxim De Cuyper alifunga bao la tatu na kuipa Brighton uongozi wa 3–2, matokeo ambayo yalidumu hadi filimbi ya mwisho na kuiondoa Manchester United kwenye mashindano.

Kwa mujibu wa Reuters, kipigo hicho kimekuwa cha kihistoria kwa United, kwani ni mara ya kwanza katika miaka 50 kupoteza mchezo wa nyumbani baada ya kuongoza kwa mabao mawili. Mara ya mwisho ilitokea Septemba 1976 dhidi ya Tottenham Hotspur.

Kocha wa Manchester United, Michael Carrick, amekubali kuwajibika kwa matokeo hayo, huku akisisitiza umuhimu wa timu hiyo kujibu kwa kiwango bora katika michezo ijayo.

Kwa upande wa Brighton, ushindi huo umeiwezesha kusonga mbele katika Carabao Cup, huku Manchester United ikiachana na matumaini ya kutwaa kombe hilo msimu huu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button