Kwingineko

Argentina yatangaza siku maalum ya kuifunga England

BUENO AIRES: SHIRIKISHO la Soka Argentina (AFA) limeidhinisha kila Julai 15 kuwa Siku ya Timu za Taifa na kuadhimisha ushindi dhidi ya England kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia 2026.

Argentina ilipindua meza kutoka bao 1-0 kwa bao la Enzo Fernandez dakika ya 85 kabla ya Lautaro Martinez kufunga la pili dakika ya 90 na Argentina kutinga fainali kwa mara ya pili mfululizo.

“Siku hii imechaguliwa maalum kwa heshima ya ushindi mkubwa na historia kwa Albiceleste (timu ya taifa Argentina) dhidi ya England kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia 2026,” ilieleza sehemu ya taarifa ya AFA baada ya kikao chao cha juzi Jumatano.

Ushindi huo wa Argentina wa Julai 15, mwaka huu pia uliibua malalamiko ya Argentina juu ya Kisiwa cha Falkland ambacho kipo umbali wa maili 8,000 mpaka England wakati kikiwa umbali wa maili 300 kutoka Argentina.

Wachezaji wa Argentina walibeba mabango yaliyosomeka: “Malvinas ni Waargentina”. Argentina wanaitambua Falkland kama Malvinas.

Hata hivyo, Argentina ilipoteza fainali kwa bao 1-0 mbele ya Uhispania na mwisho wa mchezo wachezaji wa timu hizo walitifuana.

Hilo limepelekea FIFA kuanza mchakato wa hatua za kinidhamu dhidi ya Leandro Paredes na Nahuel Molina pamoja na kocha msaidizi, Roberto Ayala.

AFA wameguswa katika uchunguzi wa masuala ya kisiasa kupitia Falkland na pia uwepo wa ubaguzi katika mchezo wa nusu fainali.

Rais wa Argentina, Javier Milei alitanabaisha shangilia ya wachezaji wakiwa na mabango ndivyo ilivyopaswa na ujumbe huo ulibeba maoni ya Waargentina wote, ingawa anafahamu FIFA itaiadhibu timu kwa faini.

Related Articles

Back to top button