Nyumbani

Msigwa: Vijana tusibaniane fursa, serikali inatuunga mkono

DAR ES SALAAM: KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amewataka vijana nchini kushirikiana na kupeana fursa badala ya kuwekeana vikwazo, akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono wale wanaotumia vipaji na ubunifu wao kuleta maendeleo.

Msigwa ametoa wito huo wakati wa hafla ya kumpongeza mtengeneza maudhui ya mtandaoni, Abdul Chacha maarufu kama Headmaster, kwa mchango wake katika kuzalisha maudhui yenye kuelimisha, kuburudisha na kujenga maadili katika jamii.

“Vijana tusibaniane, tupeane fursa kwa sababu Serikali ipo, inaona na itaendelea kutusapoti. Kikubwa ni kufanya kazi kwa bidii, ubunifu na kuonyesha uwezo wetu,” amesema Msigwa.

Amebainisha kuwa sekta ya ubunifu imeendelea kuwa chanzo muhimu cha ajira na maendeleo ya uchumi, huku akiwasihi vijana kutumia vipaji vyao kwa njia chanya na kuendelea kuzalisha maudhui yenye manufaa kwa jamii.

Aidha, ameipongeza kazi inayofanywa na Headmaster, akisema imekuwa mfano mzuri wa jinsi ubunifu unavyoweza kutumika kuelimisha na kugusa maisha ya Watanzania wengi kupitia majukwaa ya kidijitali.

Related Articles

Back to top button