Nyumbani

Fei Toto bado yupo Yanga-Walter

MENEJA wa Yanga, Walter Harrison amewataka mashabiki wa timu hiyo kupuuza uvumi unaomhusisha kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ kujiunga na Azam kwani bado yupo sana Jangwani.

Akizungumza na SpotiLeo, Meneja huyo amesema Feisal ni miongoni mwa nyota 22 waliopo kambini kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Disemba 25 dhidi ya Azam.

“Mashabiki wetu wasiyumbishwe na maneno ya mitandaoni, Feisal tupo naye kambini na kesho ni miongoni mwa wachezaji watakaoanza dhidi ya Azam, hayo ni maneno ya kuwadhoofisha ili wasije uwanjani,” amesema Walter.

Amesema Yanga ni timu kubwa na ina kikosi kipana hivyo hata kama ikitokea mchezaji huyo akiondoka haoni kama inaweza kutetereka.

Kumekuwa na uvumi mitandaoni kuwa Feisal amevunja mkataba na kuilipa Yanga Sh milioni 112 ikiwa ni malipo ya kuvunja mkataba wa muda uliobaki na fedha ya usajili wake.

Related Articles

Back to top button